1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makampuni yashutumiwa kuharibu misitu ya Kongo

9 Juni 2015

Kundi moja la Kampeni limeshtumu makampuni makubwa ya uvunaji magogo kwa kuvunja utaratibu wa sheria ya nyara za misitu ya Kongo, na kudhoofisha juhudi za kuulinda msitu wa pili mkubwa wa mvua duniani.

Bildergalerie Artenvielfalt Deutschland
Picha: picture alliance/blickwinkel

Shirika la Global Witness lenye makao yake mjini London limesema katika ripoti yake kuwa biashara ya kupasua mbao ya thamani ya kiasi cha Euro milion 87 nchini Congo hazizingatii sheria za kimataifa kuhusu uuzaji wa mbao.

Zaidi ya nusu ya bonde la Kongo lenye hekta milioni 500 za msitu ziko katika Congo taifa ambalo linajivunia kuwa nchi ya tano duniani yenye misitu mikubwa iliyo na wanyama pori na mimea mbali mbali.

Mwenyekiti wa Jopo la Maendeleo ya Afrika Kofi AnnanPicha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Biashara ya mbao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikizongwa kwa muda mrefu na ufisadi na sheria dhaifu. Ili kujaribu kushughulikia tatizo hilo,serikali ya Congo ilipitisha sheria mwaka 2002 ya kudhibiti utoaji wa leseni mpya kwa viwanda vya kupasua mbao zinazotaka kuhudumu nchini humo.

Hata hivyo, Global Witness ilisema kuwa uharibifu wa misitu ya Kongo unatokana na uvunaji haramu na hali inazidi kuwa mbaya, na kutishia viumbe hai kama tembo wa msituni na okapi, mnyama adimu anaefana na twiga na mwenye mistari kama ya pundamilia.

Kiongozi wa kampeni ya Global Witness Alexandra Pardal, alisema katika taarifa kuwa walifahamu kuwa makampuni ya uvunaji mbao yanavunja sheria za Kongo, lakini uvunjaji huo wa sheria uko katika kiwango cha kutisha.

Ripoti inatathimini uchunguzi uliofanywa juu ya mikataba 28 kati ya 57 ya viwanda vya magogo nchi hiyo ya Kongo kwa mwaka 2011 na 2014.Kila uchunguzi ulionesha shughuli za uvunjaji wa sheria ikiwa na pamoja ukataji wa magogo nje ya sehemu zinazoruhisiwa, ukataji mkubwa wa miti na kugudungulika kwa hati bandia.

Okapi ni mmoja wa wanyama wanaohofiwa kutoweka kwenye misitu ya KongoPicha: cc-by-sa-3.0/Raul654

Ripoti ya shirika hilo inayatuhumu makampuni makubwa mawili,yenye makao yake nchini Congo SIFORCO na SODEFOR,Kampuni tanzu ya Nordsudtimber ya nchini Liechtenstein, kuwa miongoni mwa wahalifu wakubwa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwa shirika la habari la Reuters, kampuni ya SODEFOR ilisema kila siku ilikuwa inafuata sheria za Kongo na inashtumiwa na shirika la Global Witness na kutakiwa kumaliza shughuli za viwanda za mbao nchini Kongo. Kampuni ya SIFORCO haikujibu barua waliyotumiwa.

Ripoti hiyo pia inaitoa dosari Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya kwa kutowekea mkazo utekelezaji wa sheria na kupiga marufuku uagizaji na kuvuna magogo kinyume cha sheria.Marekani na nchi za Ulaya zimeingiza euro milion 19.8 kutokana na mbao za Kongo mwaka 2014,kulingana na takwimu za forodha.

China inakadiriwa kununua asilimia 56 ya mbao za Kongo mwaka jana, zenye thamani ya Euro Milion 56. Jopo la Maendeleo ya Afrika, chini ya mwenyekiti wake aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, lilisema mwaka jana kuwa Afrika inapoteza zaidi ya dola bilion 17 kila mwaka kutokana na ukataji holela wa Mbao.

Mhandishi:Salma Mkalibala/RTRE

Mhariri: Iddi Ssessanga