1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gachagua asema wanafunzi 70 hawajulikani walipo

6 Septemba 2024

Makamu wa rais nchini Kenya Rigathi Gachagua amesema wanafunzi 70 hawajulikani walipo baada ya kisa cha moto kwenye bweni la shule ya msingi ya Hillside Endarasha Academy iliyoko kaunti ya Nyeri.

Kenia Nyeri | Feuer in der Hillside Endarasha Primary School
Wazazi wakikusanyika nje ya shule ya msingi ya Hillside Endarasha Academy baada ya mkasa wa motoPicha: Simon Maina/AFP

Gachagua hata hivyo amesema idadi hiyo haimaanishi wanafunzi hao 70 wamekufa ama wamejeruhiwa.

Amewaambia waandishi wa habari nje ya shule hiyo iliyoko kaunti ya Nyeri.

Soma pia: Wanafunzi 17 wafariki kwa kuteketea moto Kenya

Wanafunzi 17 wamekufa kufuatia kisa hicho na taarifa za jeshi la polisi zimesema moto huo uliwaka usiku wa manane watoto hao wakiwa wamelala.

Wanafunzi kadhaa wamejeruhiwa na 16 kati yao wamepata majeraha makubwa na wanatibiwa hospitalini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW