1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Makao makuu ya meli za Crimea yashambuliwa

22 Septemba 2023

Shambulizi la kombora la Ukraine limepiga makao makuu ya jeshi la majini la Urusi la Bahari Nyeusi kwenye rasi iliyoinyakua ya Crimea.

Crimea
Ukraine ilifanya shambulizi kali la kombora Ijumaa kwenye makao makuu ya Meli ya Bahari Nyeusi ya Urusi na askari mmoja alikosekana.Picha: Crimean Telegram channel via AP Photo/picture alliance

Shambulizi la kombora la Ukraine limepiga makao makuu ya jeshi la majini la Urusi la Bahari Nyeusi kwenye rasi iliyoinyakua ya Crimea.

Gavana wa rasi hiyo Mikhail Razvozhayev amesema hayo, huku jeshi la Ukraine pia likikiri kufanya shambulizi hilo.

Habari zaidi: Ukraine yashambulia uwanja wa ndege wa kijeshi huko Crimea

Mwanajeshi mmoja wa Urusi bado hajulikani aliko baada ya kutokea shambulizi hilo.

Hayo yamejiri mnamo wakati rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wameukomboa mji wa Bakhmut na miji mingine miwili.

Zelensky alisema hayo alipozungumza na kituo cha utangazaji cha CNN muda mchache kabla kuondoka kuelekea Canada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW