1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Makazi ya waziri mkuu wa Libya yashambuliwa

1 Aprili 2024

Makazi ya waziri mkuu wa Libya Abdulhamid al-Dbeibah yalishambuliwa Jumapili kwa mabomu katika tukio ambalo halikusababisha majeruhi

Waziri mkuu wa Libya Abdul Hamid Mohammed Dbeibah akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari mjini Tripoli mnamo Septemba 15, 2021
Waziri mkuu wa Libya Abdul Hamid Mohammed DbeibahPicha: Hazem Ahmed/AP Photo/picture alliance

Raia wawili mjini Tripoli wamesema walisikia milipuko mikubwa karibu na bahari ya eneo la kifahari la Hay Andalus mjini humo ambalo ni makazi ya Dbeibah.

Soma pia;Viongozi wakuu wa Libya wakubaliana kuunda serikali mpya

Raia mwengine ameongeza kuwa baada ya milipuko hiyo kusikika, vikosi vya usalama vilipelekwa katika eneo hilo.

Waziri mmoja athibitisha kutokea kwa shambulizi hilo

Waziri aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, alithibitisha kupitia ujumbe kwamba shambulizi hilo lilisababisha uharibifu mdogo tu bila ya kutoa maelezo zaidi.

Libya imezongwa na machafuko tangu mwaka wa 2011 baada ya kuzuka kwa uasi ulioungwa mkono na jumuiya ya kujihami ya NATO pamoja na kugawanyika kwa taifa hilo mwaka 2014 kati ya tawala pinzani za Mashariki na Magharibi, kila moja ikiungwa mkono na safu ya wanamgambo na serikali za kigeni.