Makombora ya Urusi yailenga Kyiv na kuua watu karibu 11
13 Juni 2023Mashambulio yaliharibu maghala na majengo ya makaazi ya tu.
Mashambulio hayo yaliyofanyika mji alikozaliwa rais Volodymyr Zelensky yamekuja wakati wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika hatua za awali za operesheni yake ya kukabiliana na Urusi. Picha zilizorushwa kwenye mtandao wa Telegram wa rais Zelenksy zimeonesha jinsi zima moto wanavyopambana kuudhibiti moto ulioharibu jengo la makaazi ya raia.
Soma Zaidi:Macron, Scholz na Duda wajadili amani ya Ukraine
Meya wa mji huo wa Kryvi Rih Oleksandr Vilkul, amesema watu 28 wamejeruhiwa.Rais Zelensky ameandika kwenye mtandao huo wa Telegram kwamba mashammbulio hayo yamewafanya na magaidi wa Urusi.
Katika hatua nyingine, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti Nyuklia IAEA, Rafael Grossi anatarajiwa mjini Kiev leo Jumanne katika ziara ambayo amepangiwa kukutana na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky lakini pia kutembelea kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na Urusi.
Hatua hiyo inakuja baada ya kuharibiwa wiki iliyopita,bwawa kubwa la karibu na kinu hicho. Shirika la IAEA siku ya Jumapili lilisema linahitaji kufika kwenye eneo hilo kutazama kiwango cha maji baada ya bwawa hilo kupoteza sehemu kubwa ya maji kutokana na uhribifu uliofanyika kwenye chanzo cha maji ya bwawa Kakhovka. Serikali ya Kiev inailaumu Urusi kwa kuhusika na uharibifu wa bwawa hilo la Kusini mwa Ukraine.