1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yashambulia kusini mwa Odesa, Ukraine

17 Septemba 2023

Urusi imefanya mashambulizi nchini Ukraine yanayohusisha ndege zisizokuwa na rubani na makombora mapema hii leo, yaliyolenga zaidi maeneo ya kusini mwa mkoa wa Odesa na kupiga kiwanda cha bidhaa za kilimo.

Meli ya mizigo ikiwasili katika bandari ya Chornomorsk tayari kuchukua nafaka, huku kukishuhudiwa mashambulizi ya Urusi karibu na Odesa.
Meli ya mizigo ikiwasili katika bandari ya Chornomorsk tayari kuchukua nafaka, huku kukishuhudiwa mashambulizi ya Urusi karibu na Odesa, Septemba 16, 2023.Picha: REUTERS

Jeshi la anga la Ukraine limesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba Urusi imefanya mashambulizi sita ya droni za Shahed zinazotengenezwa Iran pamoja na makombora 10.

Lakini jeshi la Ukraine lilifanikiwa kudungua droni sita na makombora sita kabla ya kuanguka kwenye maeneo yaliyolengwa. 

Hali kwenye mkoa wa Odesa na bandari zake imekua ikifuatiliwa kwa karibu na wanunuzi wa nafaka baada ya Kyiv kusema jana Jumamosi kwamba meli zenye shehena za nafaka zimewasili mkoani humo zikitumia ujia wa muda kufika kwenye bandari za Bahari Nyeusi ili kuzisafirisha kuelekea Afrika na Asia. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW