Makubaliano ya amani ya Burundi kuanza kazi kesho jumapili
9 Septemba 2006Matangazo
Makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya serikali ya Burundi na waasi wa FNL,yataanza kufanya kazi kuanzia kesho.Makubaliano hayo yanatzungumzia juu kuwekwa chini silaha na kujumuishwa waasi katika jeshi la taifa la Burundi.Hayo ni kwa mujibu wa nakala ya waraka huo uliotiwa saini alkhamisi ,na kulifikia shirika la habari la Ufaransa AFP.Mada nyengine kadhaa zinazohusiana na makubaliano ya amani ikiwa ni pamoja na muundo wa jeshi jipya la taifa huenda zikajadiliwa mazungumzo yatakapoitishwa tena,wiki moja kutoka sasa nchini Afrika kusinji.Hayo ni kwa mujibu wa mwanadiplomasia mmoja aliyeshiriki katika mazungumzo ya Daresalam.