Makubaliano ya awali kuhusu mradi wa Bwawa la Mto Nile
Oumilkheir Hamidou
16 Januari 2020
Maafisa wa serikali za Misri, Ethiopia na Sudan wanasema wamefikia hatua muhimu kuelekea makubaliano kuhusu mradi mkubwa wa bwawa katika mto Nile, mradi uliokuwa ukizusha mivutano tangu miaka tisa iliyopita.
Matangazo
Mawaziri wa mambo ya nchi za nje na maafisa wa sekta ya maji kutoka nchi hizo tatu wamekamilisha mazungumzo ya siku tatu mjini Washington pamoja na waziri wa hazina wa Marekani Steven Mnuchin na mwenyekiti wa benki kuu ya dunia Davis Malpass.
Mradi huo uliopewa jina " Bwawa kubwa la Machipuko Ethiopia" umekamilika kwa takriban asili mia 70 na unatoa matumaini ya kukidhi mahitaji makubwa ya nishati kwa wakaazi zaidi ya milioni 100 wa Ethiopia. Hata hivyo, maafisa wa Misri wanahofia mradi wa bwawa hilo usije ukapelekea kupungua kiwango cha maji yanayohitajika nchini Misri.
Taarifa ya pamoja iliyochapishwa mjini Washington haikutoa maelezo ya muda gani utahitajika kuweza kujaza bwawa hilo, imesema tu tukio hilo litafanyika hatua kwa hatua katika msmu wa mvua ambao kawaida ni kati ya Julai hadi Agosti. Mapema mwezi huu waziri wa maji na nishati wa Ethiopia, Sileshi Bekele alisema nchi yake inataka kipindi cha miaka 12 cha kujaza bwawa hilo huku Misri ikidai kipindi cha miaka 21.
Majadiliano ya wiki hii yalilengwa kubuni kanuni na muongozo wa jinsi ya kupunguza kishindo kinachoweza kusababishwa na hali ya ukame na viwango ya maji katika bwawa hilo.
"Mawaziri wanakubaliana kwamba nchi zao tatu zina jukumu la pamoja katika kusimamia matatizo ya ukame" maafisa hao wamesema katika taarifa yao.
Mradi wa bwawa la kuzalisha umeme Ethiopia
Kazi katika mradi wa bwawa la maji la kuzalisha umeme huko Ethiopia imeshika kasi huku jaribio la kuutatua mgogoro wa Ethiopia na nchi jirani zinazopakana na mto Nile zikiendelea.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Matarajio makubwa (52002200)
Hapa ndipo lilipoundwa: Bwawa kubwa ambalo linatarajiwa kutoa umeme wa kutosha kwa Ethiopia na majirani zake. Dola bilioni tano za kimarekani. Mradi huu unaotarajiwa kuanza kuzalisha umeme kuanzia mwaka 2022 utagharimu dola bilioni nne za kimarekani. Ni mradi mkubwa lakini umesababisha pia mgogoro wa kidiplomasia kati ya Misri na Sudan kwani nao wanategemea maji ya mto Nile.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Jengo kubwa lililojengwa kwa Sementi (52002162)
Ni bwawa lenye urefu wa mita 145, karibu kilometa 2. Eneo lake la ujenzi lina kiometa saba za mraba. Ethiopia inasubiri kwa hamu kukamilika kwa ujenzi. Takribani nusu ya kaya nchini humo kwa sasa hazina umeme. Jengo hili linaweza kuboresha hali za kaya hizo. Nchi hii inataka kuuza sehemu ya umeme utakaotokana na mradi huu nchi jirani.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Eneo kubwa kugeuka kuwa ziwa (52002187)
Ili maji yazalishe umeme wa kutosha ni lazima bwawa litengenezwe. Mhandisi Abdu Yibera anasema Ndani ya “miaka michache eneo hili litajaa maji”. Bwawa hio linasemekana kuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za mraba bilioni 74 za maji. Ethiopia inataka kulijaza maji ziwa hili la lutengenezwa mapema iwezekanavyo lakini nchi jirani zinasita kufanya hivyo.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Mzozo kati ya nchi za Nile
Ethiopia inapanga kujaza hifadhi hiyo ya maji ndani ya miaka saba. Misri yenyewe inasema ni miaka 21. Inaogopa kuwa kiwango cha maji katika mto Nile kitashuka kwa haraka wakati Ethiopia itakapoanza kulitumia bwawa hilo. Iwapo kutakuwa na uhaba wa maji ama ukame, Ethiopia inapaswa kuihakikishia Misri upatikanaji wa maji. Majadiliano yote na majaribio ya usuluhishi hayajawa na mafanikio hadi sasa.
Suluhisho liko wapi?
Wakati wa ziara yake Afrika ya Kusini, Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alimwomba Rais Cyril Ramaphosa kusaidia. Anatajwa kuwa msuluhishi kwenye mgogoro wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Misri. Ramaphosa atakuwa mwenyekiti wa AU mwezi huu kama ilivyo kawaida ya mzunguko wa kiti hicho: Abiy hawezi kumuomba usaidizi mwenyekiti wa sasa wa Umoja huo kwani kiti hicho kinakaliwa na Rais wa Misri.
Picha: AFP/P. Magakoe
Kazi inaendelea wakati joto likiwa nyuzi Jjto 50
Wakati majadiliano yakiendelea kazi katika eneo la ujenzi inaendelea. Watu 6000 wanafanya kazi wakati wote, mara nyingi kukiwa na joto lisilo la kawaida. Wakati wa miezi yenye joto kali, viwango hupanda hadi nyuzi joto 50
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Mtambo wa kuzalisha umeme hapo baadaye
Mashine za kuchomelea zinafanya kazi. Hatua inayofuata ni kuzipanga sehemu mbili za injini katika moja ya mitambo miwili ya kuzalisha umeme. Maandalizi yamekamilika. Injini za kwanza zinatarajiwa kuwa tayari kwa matumizi katikati mwa mwaka 2021
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Uendeshaji wa mradi mkubwa
Injini zitafungwa hapa. Jumla ya Uniti 13 zimepangiwa na kugawanywa katika mitambo miwili kwenye kingo zote. Mitambo ya kuzalisha umeme ya bwawa kubwa la Ethiopia inatarajiwa kutoa gigawati 15,000 za umeme kwa mama. Mtambo huo utakuwa na nguvu zaidi kuliko mitambo mingine ya kuzalisha umeme barani Afrika.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Tuhuma na Ucheleweshaji
Bwawa lilitakiwa liwe limeshakamilika. Lakini usimamizi mbaya na tuhuma za rushwa zimerefusha hatua ya ujenzi. Sehemu ya kwanza ilikamilika mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita: Ukuta wa bwawa umelalia upande mwingine wa Ethiopia na unafunga eneo linalotumika kuzuia maji.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Matarajio
Maji yanafuata mkondo wake kuingia kwenye bwawa. Mto wa Blue Nile unatiririka toka hapa kuelekea Sudan na Misri. Ni kwa kiasi gani mkondo huu utawafikia watu hapo baadaye itategemea namna majadiliano na usuluhishi utakavyokuwa kati ya Misri na Ethiopia.Kwa vyovyote vile, Misri tayari imeshatangaza kuwa inataka kununua umeme wa Ethiopia.
Picha: DW/M. Gerth-Niculescu
Picha 101 | 10
Makubaliano timamu huenda yakatiwa saini january 28 na 29 mjini Washington
Taarifa hiyo imeongeza kusema makubaliano ya awali kuhusu shughuli za bwawa hilo hayatokamilika hadi pale nchi husika zitakapokubaliana kuhusu vifungu vyote vya mivutano. Wawakilishi wa nchi hizo tatu wanapanga kukutana tena January 28 na 29 inayokuja mjini Washington lengo likiwa kufikia makubaliano ya mwisho kuhusu namna ya kujaza na kusimamia shughuli za bwawa hilo.
Itafaa kusema hapa kwamba bwawa hilo kubwa lenye urefu wa kilomita moja nukta nane linalokenda juu mita 145 limeanza kujengwa tangu mwaka 2012 na Etrhiopia. Mradi huo mkubwa wa mabilioni ya dala unatarajiwa kuanza kutoa umeme ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2020 na kukamilisha shughuli zake mwaka 2022. Linasifiwa kuwa bwawa kubwa kabisa barani Afrika likiwa na uwezo wa kuzalisha Megawat 6000 za umeme.