1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Makubaliano ya kusitisha mapigano DRC yavunjika

21 Oktoba 2024

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa yamevunjika baada ya kuanza mapigano mapya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanajeshi wa Kongo
Wanajeshi wa KongoPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa yamevunjika baada ya kuanza mapigano mapya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.

Duru za eneo hilo zimeeleza kuwa alfajiri ya jana Jumapili, waasi wa M23 walipambana na wanamgambo wa Wazalendo. Raia 14 wamejeruhiwa wakiwemo vijana wawili.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalifikiwa kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda  na yalianza mapema mwezi Agosti chini ya upatanishi wa Angola. Wakati huo huo mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yalikwama, lakini duru mpya ya mazungumzo imepangwa kufanyika mjini Luanda mwishoni mwa wiki ijayo.