Makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza karibuni kufikiwa
24 Januari 2024Matangazo
Qatar, Marekani na Misri zimekuwa zinafanya juhudi za kidiplomasia tangu mwezi Desemba ili kupunguza tofauti kati ya Israeli na Hamas kwa lengo la kuondosha uhasama, ili kuwezesha misaada zaidi ya kibinaadamu kupelekwa katika Ukanda wa Gaza.
Hata hivyo, pande hizo mbili bado zinatofautiana jinsi ya kuvimaliza kabisa vita vya Gaza, lakini Hamas imekataa kusonga mbele bila ya suala hilo kutatuliwa.
Msemaji wa serikali ya Israel, Eylon Levy, amesema hakuna hatua ya kusimamisha mapigano itakayochukuliwa ambayo itawaachia Hamas waendelee kuwamo madarakani kwenye Ukanda wa Gaza na bila ya kuachiwa mateka wa Israel.