1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Makubaliano ya kisitisha vita Syria yarefushwa kwa siku 15

25 Januari 2026

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya mpito ya Syria na wapiganaji wanaoongozwa na wanamgambo wa Kikurdi (SDF) yamerefushwa kwa siku 15. Ni baada ya makubaliano ya awali yaliyofanyika Jumanne kuisha muda.

Jeshi la Syria limepata udhibiti wa sehemu kubwa ya maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na wapiganaji wa Kikurdi
Jeshi la Syria baada ya kupata udhibiti wa eneo la Maskanah.Picha: Izz Aldien Alqasem/Anadolu Agency/IMAGO

Wizara ya Ulinzi ya Syria imesema uamuzi huo unakusudia kuwezesha mchakato wa kuwahamisha wanamgambo wenye itikadi kali wanaoshikiliwa kwenye magereza kaskazini mashariki mwa Syria na kuwapeleka Iraq.

Mchakato wa kuwahamisha waliofungwa kwenda Iraq waanza

Vikosi vya Marekani vimeshaanza kuwahamisha wanamgambo hao wanaodaiwa kuliunga mkono kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS). Katika wiki za karibuni, serikali ya Syria imekuwa ikipambana dhidi ya maeneo hayo yaliyokuwa yakidhibitiwa na wanamgambo wa Kikurdi na imefanikiwa kuyadhibiti kwa kiasi kikubwa.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW