1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano kusitishwa Pakistan baada ya watu 82 kuuliwa

Josephat Charo
25 Novemba 2024

Pakistan ina idadi kubwa ya waumini wa madhehebu ya Sunni, lakini wilaya ya Kurram katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, karibu na mpaka na Afghanistan, ina idadi kubwa ya waumini wa madhehebu ya Shia.

Watu wakiomboleza kwenye makaburi ya jamaa zao waliouwawa baada ya watu wenye bunduki kuyashambulia magari ya abiria wilaya ya Kurram, mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa
Watu wakiomboleza kwenye makaburi ya jamaa zao waliouwawa baada ya watu wenye bunduki kuyashambulia magari ya abiria wilaya ya Kurram, mkoa wa Khyber PakhtunkhwaPicha: REUTERS

Maafisa wa Pakistan wametangaza siku saba za usitishaji mapigano baada ya mapambano makali ya risasi kati y amakabila katika wilaya ya Kurram, kaskazini magharibi mwa nchi, ambayo yamesababisha watu kiasi 82 kuuwawa na wengine 156 kujeruhiwa.

Msemaji wa serikali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, Muhammad Ali Saif, amesema pande hizo mbili zimeafikiana kuhusu kusitisha mapigano kwa siku saba, ambapo wakati wa kipindi hicho watabadilishana wafungwa na kukabidhiana maiti za watu wao waliouwawa.

Afisa wa eneo hilo amesema juhudi zinafanywa kuwarejesha watu 20 ambao waliokuwa hawajulikani waliko pande zote mbili.

Machafuko yalizuka Alhamisi iliyopita wakati misafara miwili tofauti ya waislamu wa madhehebu ya Shia iliyokuwa ikisindikizwa na polisi iliposhambuliwa na waumini wapato 43 kuuwawa, na kuzusha makabiliano ya risasi ya siku mbili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW