1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya matumizi ya maji ya Nile yaanza kutekelezwa

15 Oktoba 2024

Ushirikiano wa kikanda wa nchi 10 umesema makubaliano kuhusu matumizi sawa ya rasilimali za maji katika Bonde la Mto Nile, yameanza kutekelezwa, licha ya upinzani kutoka Misri.

Misri | Mto Nile
Mto Nile unapitia mataifa kadhaa ya Afrika kabla ya kufika Misri.Picha: Schoening/picture alliance

Ushirikiano wa kikanda wa nchi 10 umesema makubaliano kuhusu matumizi sawa ya rasilimali za maji katika Bonde la Mto Nile, yameanza kutekelezwa, licha ya upinzani kutoka Misri. 

Mkataba wa kisheria wa mfumo wa ushirika, ulithibitishwa rasmi na Umoja wa Afrika baada ya Sudan Kusini kujiunga, na ulianza kutumika Jumapili. 

Ethiopia, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania zimeridhia makubaliano hayo. 

Soma pia: Makubaliano ya awali kuhusu mradi wa Bwawa la Mto Nile

Misri na Sudan zimekataa kusaini, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikijizuia. Kenya bado haijawasilisha katika Umoja wa Afrika, nyaraka zake za uidhinishaji. 

Taarifa iliyotolewa na Mpango wa Bonde la Mto Nile, imeeleza kuwa makubaliano hayo ni ushahidi wa azimio lao la pamoja la kutumia Mto Nile kwa manufaa ya wote, kuhakikisha matumizi yake ni sawa na endelevu kwa vizazi vijavyo. 

Hatua ya Misri na Sudan kutosaini mkataba huo, inamaanisha kuwa makubaliano hayo yatakuwa yenye utata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW