1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Makubaliano ya usalama ya DRC na Rwanda kuanza Oktoba

25 Septemba 2025

Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda zimekubaliana kuanza utekelezaji wa hatua za kiusalama mwezi ujao chini ya makubaliano yaliyoratibiwa na Marekani.

USA Washington D.C. 2025 | Donald Trump akiwa na hati yamakubaliano ya amani kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mawaziri wa mambo ya nje wa DRC Thérèse Kayikwamba Wagner(kulia) na Rwanda Olivier Nduhungirehe(kushoto) pamoja na Rais TrumpPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP/Getty Images

Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda zimekubaliana kuanza utekelezaji wa hatua za kiusalama mwezi ujao chini ya makubaliano yaliyoratibiwa na Marekani. Tangazo hilo limetolewa katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano, katika kile ambacho kitakuwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa makubaliano hayo ya amani huku kukiwa na wasiwasi juu ya maendeleo yake.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa katika mkutano wa Washington Septemba 17-18na kuripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Reuters, yataanza Oktoba 1, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja, ambayo pia ilitolewa na Marekani, Qatar, Togo na Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Nchi hizo zilikubali kukamilisha hatua hizo ifikapo mwisho wa mwaka, vyanzo vitatu vinavyofahamu suala hilo viliiambia Reuters. Kongo na Rwanda pia bado hazijapanga tarehe kwa wakuu wa nchi kusafiri kwenda Washington huku mazungumzo ya Doha, yakisuasua.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW