Makubaliano yafikiwa Somalia kuhusu uchaguzi uliocheleweshwa
26 Mei 2021Matangazo
Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Somalia Mohammed Abdirizak amesema makubaliano kuhusu masuala matatu muhimu ya kukamilisha mkataba huo yamefikiwa kimsingi jana, kufuatia kuhitimishwa kwa mazungumzo yaliyoanza Mei 22 kati ya serikali ya shirikisho na majimbo.
soma zaidi: Bunge la Somalia labatilisha nyongeza ya muhula wa Rais
Amesema tamko linaloeleza kwa kina makubaliano hayo litatolewa Alhamisi katika hafla ya kuhitimishwa rasmi.
Kumekuwa na shinikizo kubwa dhidi ya Rais Mohamed Abdullahi Mohamed baada ya uchaguzi uliopangwa Februari nane kushindwa kufanyika kwa sababu ya kukosekana kwa makubaliano ya jinsi uchaguzi huo unapaswa kuandaliwa.