1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAKUMBUSHO YA HOLOCAUST BERLIN NDIO MADA KUU GAZETINI:

11 Mei 2005

Tukianza na gazeti la BERLIN la TAGESSPIEGEL- linakumbusha mjadala motomoto uliodumu mwaka mzima humu nchini kuhusu makumbusho hayo:

Laandika:

“Jengo la makumbusho kwa wayahudi waliouliwa barani Ulaya na mjadala wake mrefu uliofuatia si zoezi baya la demokrasia.Kwani ni katika utawala wa kidikteta tu ndio azimio la kujenga ukumbusho wowote unapitishwa kimabavu.Utawala wa miaka 12 wa Manazi,miaka 7 ya mvutano juu ya umbo na sura ya makumbusho hayo ni muda uliohitajika kujenga msingi wa makumbusho yatakayowazindua watu siku za mbele kilichotendeka.Endapo mtu leo akizingatia barabara walioungamkono ujenzi wa makumbusho na waliopinga kile alichojenga Peter Eisenman,hana budi kustaajabu kwa ufanisi wake.”-lamandika DER TAGESSPIEGEL .

Katika gazeti la MITTELDEUTSCHEN ZEITUNG linalochapishwa mjini Halle tunasoma:

„Ni vyema sasa baada ya patashika iliozuka sasa tuna kituop hiki cha makumbusho.Ni vyema pia kwamba makumbusho hayo yamejengwa katika kitovu cha jiji la berlöin kwa kila mmoja kuyaona.Kule ambako mabingwa wa Kinazi wa mikakati ya njama ya kuwahilikisha binadamu wenzao makumbusho hayo ndiko yaliko.

Kule ambako baada ya vita vya dunia na vita baridi sasa kumeibuka mji mkuu uliofunua macho na kukaribisha walimwengu.Hii imewezekana si kwa urahisi.Fikra na rai hutokana na kuelewa kilichotendeka, kuona aibu,kujitwika dhamana kwa madhambi yasiofutika dhidi ya ubinadamu na kuonesha huzuni kwa wahanga .Kwa njia hii, makumbusho hayo yatakisaidia kizazi cha waliofanya madhambi ya kuhilikishwa kwa wayahudi wa Ulaya kufahamu nini hasa kilichopita..“

Katika gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN tunasoma kwamba, mabishano,ugomvi na makosa –yote yaligubika ujenzi wa makumbusho haya.Kustaajabu kwanini ikawa hivyo, ni kosa.Kwani, haikuwahi kutokea kabla huku Ujerumani msiba muovu kama ule wa kuhilikishwa umma wa wayahudi kukumbushwa watu kwa aina ya jengo la sanaa. Sasa makumbusho hayo yamesimama kila mmoja aone.“

Gazeti la OSTSEEZEITUNG linajishughulisha naila juu ya jengo hilo:

Alama hii yenye sura ya makaburi tayari imezusha maoni tofauti.Baadhi wanadai hayana maana yoyote, hayakuhitajika na baridi.Je,hayana maana kama mauaji yenyewe ya wayahudi milioni 6 ?-lauliza gazeti.Likendelea, OSTSEE ZEITUNG lauliza zaidi: Hayakuhitajika kama mipango ya umangimeza kuhilikisha umma wa watu ?

Je, ni baridi kama kambi za wafungwa za Auschwitz,Majdanek na Treblinka ?

Kuna wengi watakaogeuza njia hapo wakienda cinema na mikahwani huko Potsdamer platz.Kwa sababu hawataki kujikumbusha madhambi ya uhalifu wa Manazi.Haya ni makumbusho,lamaliza gazeti, ambayo mtu hawezi kukituliza kichwa chake na kustarehe.

Mwishoe, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linatugeuzia mada likichambua ziara ya rais George Bush nchini Georgia:Laandika:

„Rais Putin atakereka kwa Bush kudai kuwa mamlaka na ardhi kamili ya Jamhuri hii ya Kaukasus yaheshimiwe.Putin anakasirishwa pia na kujitandaza zaidi kwa Marekani katika eneo hilo,kwani anakuangalia kama changamoto katika mashindano ya kuania ushawishi.Lakini,kwanza Putin hawezi na pili mpenda madaraka huyu ni mwerevu vya kutosha kufahamu kwamba kuwapo nchi za kidemokrasi karibu na mipaka yake Russia ni bora kuliko kuwa na nchi za wasi wasi ambazo Russia ingezitumia kueneza mamlaka yake kwa gharama kubwa ili kuzichezea itakavyo………“

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW