1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMyanmar

Makumi ya Warohingya waokolewa baharini wakikimbia madhila

21 Machi 2024

Maafisa nchini Indonesia wamewaokoa karibu wakimbizi 69 waliokwama baharini kwa wiki kadhaa na kuwapeleka ufukweni baada ya boti yao kupinduka.

Indonesia | Rohingya
Warohingya wengi hutumia boti za mbao na mitumbwi kukimbia madhila nchini Myanmar.Picha: Riska Munawarah/REUTERS

Boti ya mbao ya wakimbizi hao na meli nyingine iliyokuwa ikijaribu kuwasaidia zote mbili zilipinduka jana Jumatano, huku manusura wakikadiria takribani Warohingya 150 walikuwemo kwenye boti hiyo na wengi miongoni mwao walizama majini.

Kundi la waokozi walikimbilia baharini kuwaokoa wakimbizi hao baada ya kuwaona wakiwa wamekwama majini, wakishikilia mabaki ya boti iliyozama karibu na pwani ya jimbo la Aceh, mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la uokozi la Banda Aceh limesema jumla ya wahanga 69 wameokolewa, 42 kati yao wakiwa ni wanaume, wanawake 18 na watoto 9.

Maelfu ya Warohingya wengi wao wakiwa Waislamu wanakimbia mateso nchini Myanmar, na wengi huondoka kupitia baharini wakijaribu kufika Malaysia au Indonesia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW