1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makumi wajeruhiwa kufuatia mapigano mashariki mwa DRC

17 Januari 2025

Makumi ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi wamelazimika kuyahama makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la Kongo na wapiganaji wa M23.

Wanajeshi wa DRC huko Masisi
Wanajeshi wa DRC huko Masisi Picha: Alain Uaykani/Xinhuaa/picture alliance

Hayo yameelezwa na vyanzo vya ndani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali. Kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, ambalo sasa linachukuliwa kama kundi la kigaidi na serikali mjini Kinshasa, limechukua udhibiti wa maeneo mengi mashariki mwa DRC, eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali na lililokumbwa na migogoro kwa miaka 30.

Soma pia: Jeshi la Kongo latangaza kuuchukuwa tena mji wa Masisi

Katika wiki za hivi karibuni, kundi hilo la waasi wa M23 limepata nguvu zaidi na mapema mwezi huu lilidhibiti mji mkuu wa eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Jeshi la Kongo limeapa kuchukua tena udhibiti wa maeneo yote na limekuwa likifanya mashambulizi ya kukabiliana na kundi hilo.

           

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW