Makundi ya kibinaadamu Somalia yatangaza ukame nchini humo
26 Aprili 2021Matangazo
Taarifa ya pamoja ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia pamoja na wizara ya masuala ya maafa na majanga imesema kwamba zaidi ya asilimia 80 ya taifa hilo inakabiliwa na ama ukame wa wastani ama mbaya kabisa.
Mvua za chini ya kiwango kwa zaidi ya miezi miwili huenda zikachochea mazingira ya ukame kuwa mabaya zaidi katika eneo kubwa la nchi hiyo.
soma zaidi:Amnesty International: Wakimbizi wa ndani nchini Somalia wakabiliwa na dhiki kubwa
Mashirika hayo ya kibinaadamu kwa pamoja yamesema yatahitaji dola bilioni 9 ili kuwasaidia watu milioni 4 wenye mahitaji.
Azimio hilo linatolewa wakati Somalia ikiwa inakabiliwa na janga la virusi vya corona, mzozo wa kisiasa na mashambulizi ya mara kwa mara ya kigaidi.