SiasaSudan
Makundi ya Sudan yaanza mazungumzo ya serikali ya mpito
10 Januari 2023Matangazo
Akizungumza jana na waandishi habari, mwanasiasa Khalid Omer Yousif, alisema kuwa lengo la matokeo ya mkutano huo ni kuwakilisha msingi mpana wa Wasudan na kueleza maoni ya wadau.
Mwezi uliopita, vyama hivyo vilisaini mkataba na jeshi kuanzisha kipindi kipya cha mpito wa kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi. Lakini waandamanaji waliyakosoa makubaliano hayo wakisema hayana uwakilishi na yaliacha masuala yenye utata kwa ajili ya mazungumzo zaidi. Mazungumzo yajayo yataangazia masuala yaliyoachwa kwenye mfumo wa makubaliano ikiwemo, kipindi cha haki cha mpito, mageuzi katika sekta ya usalama, mpango wa amani uliosainiwa mwaka 2020 na mivutano mashariki mwa Sudan.