Makundi ya wahalifu nchini Ecuador yaharibu daraja
2 Septemba 2023Kamanda wa idara ya taifa ya Polisi Luis Garcia, ameliambia shirika la AP kwamba mlipuko wa karibuni zaidi wa baruti, ulitokea mapema jana kwenye daraja linalounganisha miji miwili katika mkoa wa Pwani wa El Oro.
Soma pia:Magenge ya uhalifu yazidi kuitikisa Ecuador
Katika kipindi hicho, mamlaka hazikuweza kuwafanya wafungwa hao kuwaachia huru zaidi ya maafisa 50 wa polisi na walinzi wote wa magereza waliowateka nyara Jumatano.
Hali ya maafisa 13 bado haijulikani
Consuelo Orellana, gavana wa jimbo la Azuay, amesema jana kwamba mateka 44 katika gereza moja mjini Cuena wameachiwa huru.
Hata hivyo mfumo wa urekebishaji tabia wa nchi hiyo na huduma ya taifa kwa watu walionyimwa uhuru hazikutoa maelezo kuhusu hali ya maafisa wengine 13 wanaoshikiliwa mateka.