1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

serikali yafikia makubaliano na makundi ya wanamgambo Libya

24 Agosti 2024

Makundi ya wabeba silaha na mamlaka za Libya, zimefikia makubaliano ya kulinda miundombinu muhimu nchini humo.

Libya
Makundi ya wanamgambo na mamlaka zafikia makubaliano ya kiusalama LibyaPicha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

 

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya Imad Trabelsi pande hizo mbili zimefikia makubaliano baada ya Umoja wa Mataifa kuonesha wasiwasi kuhusu mapigano ya hivi karibuni na mzozo unaoihusu benki kuu ya nchi hiyo.

Gavana wa benki hiyo Seddik Seddik al-Kabir, amekuwa akikosolewa na watu wa karibu na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah kuhusu usimamizi wa rasilimali za mafuta na bajeti ya serikali.

Walibya wanataka mipasuko ikome mna uchaguzi ufanyike nchini mwao

Jumapili iliyopita, mkuu wa kitengo cha tehama cha benki hiyo alitekwa nyara kwa muda na kundi la wabeba silaha ambalo halikutambuliwa, hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli za taasisi hiyo hadi alipoachiliwa. 

Libya imekuwa ikipambana kujiimarisha baada ya miaka mingi ya mzozo baada ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moamer Ghadafi kuondolewa madarakani. 

Hadi sasa taifa hilo linakabiliwa na mgawanyiko kati ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa inayoongozwa na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah, na utawala ulio upande wa mashariki unaoongozwa na Khalifa Haftar.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW