Makundi ya Wapalestina yatangaza siku ya Ghadhabu
28 Juni 2020Makundi ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza yamesema yanatekeleza siku ya ghadhabu leo Jumapili kupinga mpango wa Israel wa kutanya kuyanyakua kwa nguvu maeneo ya Wapalestina katika ukingo wa Magharibi yanayokailiwa na Israe.
Vipeperushi vilivyoandaliwa kwa pamoja na makundi ya kiislamu na makundi ya wanamgambo walioko Gaza vimewatolea mwito Wapalestina kushiriki kwenye tukio hilo litakalohudhuriwa na makundi yote ya Palestina pamoja na viongozi wa kisiasa katika ukanda wa Gaza Julai mosi.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na serikali yake ya mseto na aliyekuwa mpinzani wake Benny Gantz anatarajiwa huenda akawasilisha mbele ya bunge na baraza lake la mawaziri, pendekezo la kunyakuliwa kwa ardhi hiyo ya Wapalestina wanayoikalia tangu mwaka 1967 baada ya vita vya siku sita .
Kwa mujibu wa Talal Abu Zarifa, mwanachama wa ngazi ya juu katika kundi la kupigania ukombozi wa wapalestina (DFLP) maandamano yatafanyika katika mji wa Gaza wakati uamuzi kuhusu ikiwa maandamano yatafanyika pia kwenye eneo la Mashariki mwa Gaza kwenye mpaka na Israel bado haujafikiwa. Kundi lenye silaha ambalo ni tawi la kundi la Hamas-la al-Qassam Brigade, limetangaza kwamba hatua ya Israel ya kuchukua kwa nguvu ardhi ya Wapalestina Ukingo wa Magjaribi itakuwa ni tangazo la vita.
Umoja wa Ulaya na Marekani limeliweka kundi la Hamas ambalo limepania kuiangamiza Israel katika orodha ya makundi ya kigaidi.
Kundi hilo la Hamas lilitwaa udhibiti wa ukanda wa Gaza mwaka 2007 kutoka mikononi mwa uongozi wa rais mwenye msimamo wa wastani Mahmoud Abbas.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Tatu Karema