MALABO : Serikali ya Equatorial Guinea yajiuzulu
11 Agosti 2006Matangazo
Waziri Mkuu Miguel Abia Biteo Borico na serikali yake nzima ya taifa la Afrika Magharibi la Equatorial Guinea imejizulu hapo jana.
Katika hotuba iliyoonyeshwa na televisheni ya taifa Abia Bite amesema wanawacha nyadhifa zao ili kwamba Rais Teodoro Obiang Nguema aweze kuingiza msukumo na nguvu mpya kwenye timu ya serikali mpya.
Obiang ambaye amekuwa akimshutumu vikali Abia Biteo katika kipindi cha miezi michache iliopita hususan kutokana na rushwa na kukosa uwezo wa kuongoza amekubali kujiuzulu huko kwa pamoja kwa serikali ambayo imekuwa madarakani tokea mwaka 2004.