JamiiMalawi
Malawi iko hatarini kushuhudia ongezeko la kipindupindu
21 Machi 2023Matangazo
Kimbunga Freddy kilisababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya maji na vyoo katika nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na wizara ya afya jana jumatatu wakati ikitowa tahadhari.Nchi hiyo tayari ilikuwa ikipambana na mripuko wa ugonjwa huo hatari wakati kimbunga hicho kilipopiga wiki iliyopita.
Soma pia: Malawi yatoa wito wa msaada wa kimataifa kufuatia kimbunga Freddy
Mripuko huo ulioanza mwaka jana umeshawathiri zaidi ya watu 30,600 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700.