1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malawi, Morocco watinga nusu fainali WAFCON

10 Agosti 2026

Malawi ambao ndio wanashiriki kwa mara ya kwanza Kombe la Mataifa Barani Afrika, WAFCON, wametinga nusu fainali ya mashindano hayo.

Nigeria wakipambana na wenyeji Morocco
Nigeria wakipambana na wenyeji MoroccoPicha: Mansa Ayoola/Shengolpixs/IMAGO

Wameilaza Ghana 2-1 hapo Jumapili na ushindi huo umewapelekea kufuzu moja kwa moja katika Kombe la Dunia mwakani.

Malawi sasa wanaungana na Algeria, Cameroon na Morocco katika nusu fainali na hizo timu nne ndizo zitakazofuzu moja kwa moja kwenye Kombe la Dunia.

Kina dada hao wa Malawi sasa watakwaana na Algeria kwenye nusu fainali itakayochezwa Jumatano.

Wenyeji Morocco watapambana na Cameroon baada ya kuushangaza ulimwengu kwa kuiondoa Nigeria ambao ndio mabingwa katika robo fainali huko Casablanca walipoichapa 1-0.

Fainali ya WAFCON itachezwa Jumapili huko mjini Rabat.

Nigeria hawajawahi kukosa kufuzu Kombe la Dunia na iwapo watakosa safari hii basi itakuwa ni historia nyengine mbaya kwa hao Super Falcons.

Wana nafasi ya kushiriki mashindano hayo kupitia mechi ya mchujo watakayocheza na Afrika Kusini Alhamis kisha Ghana wavaane na Ivory Coast. Washindi wa mechi hizo mbili wataelekea kucheza mechi za mchujo za mabara ili kufuzu Kombe la Dunia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW