Asili na mazingiraMalawi
Malawi yapokea fidia ya dola mil.11 za athari za ukame
20 Agosti 2024Matangazo
Kitita hicho kimelipwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika baada ya nchi hiyo kutangaza ukame kuwa janga la taifa mapema mwaka huu.
Fedha hizo zitasaidia kutoa chakula kwa kaya zipatazo laki 235,000 katika mikoa iliyoathirika zaidi na ukame.
Aidha pia, Benki ya Maendeleo ya Afrika imesema zaidi ya kaya laki 100,000 zitanufaika na msaada wa malipo ya moja kwa moja.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameyataja malipo hayo kuwa ni njia ya kuokoa maisha ya watu wanaoishi katika mazingira magumu nchini Malawi.
Mvua zilizonyesha kati ya mwezi Novemba na Aprili zikiambatana na hali ya El Nino zimechangia mazao kushindwa kustawi katika eneo la kusini mwa Afrika.