1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malawi yarudia kura ya urais

23 Juni 2020

Malawi inarudia uchaguzi wa rais Jumanne leo baada ya korti kuyafuta matokeo ya mwaka 2019 ambayo Rais Peter Mutharika alishinda. Washindani wakuu kwenye uchaguzi huo ni Rais Mutharika na Dr. Lazarous Chakwera.

Malawi | Wahlkampf | Wahlen | Coronavirus |
Picha: Getty Images/AFP/A. Gumulira

Katika uchaguzi mkuu wa rais nchini Malawi mwaka uliopita, Rais Peter Mutharika wa chama tawala cha Democratic Progressive, DPP, alimshinda kwa asilimia ndogo, Lazarus Chakwera, mgombea anayeungwa mkono na muungano wa vyama vya upinzani, kikiwemo chama cha Malawi Congress na United Transformation Movement. Upinzani uliwasilisha kesi katika mahakama ya kikatiba kuyapinga matokeo hayo ukidai ulikumbwa na visa vya udanganyifu.

Mahakama hiyo iliyafuta matokeo hayo. Mahakama ya juu pia ikafanya uamuzi sawa na huo, huku jaji mkuu Frank Kapanda akisema visa vya udanganyifu vilivyotokea vilikuwa vikubwa, na kuitaja rufaa iliyowasilishwa na Rais Mutharika kuwa ya kuaibisha.

Vuguvugu la kutetea haki za binadamu HRDC, limekuwa likiongoza maandamano kushinikiza mabadiliko nchini Malawi. Gift Trapence ambaye ni kiongozi wa vuguvugu hilo amesema uchaguzi mpya utawapa nguvu Wamalawi.

Malawi: Mahakama yatupilia mbali ombi la Mutharika

"Tumeona idara yetu ya mahakama ikiwa huru na kufanya maamuzi muhimu hasa kuhusu uchaguzi na pia kuhusu maandamano ambayo Wamalawi wamekuwa wakifanya. Kwa hivyo demokrasia yetu inazidi kukua na Wamalawi pia wanapata nguvu. Wanajua haki zao, na watu wamekuwa wakisimama upande mzuri wa demokrasia. Kwa hivyo kama nchi nafikiri tuko katika mwelekeo sawa." Amesema Trapence.

Waandamanaji mjini Lilongwe Malawi (Aprili 27, 2019, wanaopinga madai ya uongozi mbaya wa Rais Peter Mutharika (Picha ya maktaba)Picha: Getty Images/AFP/A. Gumulira

Mnamo mwaka 2019, kulitokea machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Malawi. Watu waliuawa, wengine walijeruhiwa na mali iliharibiwa.

Waandamanaji walimshutumu mwenyekiti wa tume ya uchaguzui nchini humo Jane Ansah pamoja na timu yake huku mahakama ikiitaja tume hiyo kuwa ilioshindwa kazi.

Rais Mutharika alimteua jaji wa mahakama kuu Dr. Chifundo Kachale kuwa mwenyekiti mpya wa tume hiyo, na ameapa kuzingatia uhuru, haki na maadili katika uchaguzi.

HRW: Malawi ihakikishe uchaguzi huru na salama

"Tutaendelea kushirikiana vyema na  vyama vyote vya kisiasa na tuendeleze mafanikio ambayo tumeshapata katika kipindi ambacho tumekuwa ofisini." Amesema Dr. Chifundo Kwachale

Katika mitaa mbalimbali Malawi, kuna matumaini kwamba uchaguzi unaorudiwa utakuwa mwanzo mpya. Owen Chimaliro ambaye ni raia wa Malawi ameeleza kuwa "Mambo mazuri yanakuja kwa sababu serikali hii imeharibu kila kitu. Kila mmoja Analia. Tunajaribu hili na lile lakini haisaidii. Kwa hivyo sasa tunasubiri mabadiliko kutoka katika serikali ijayo na tuna matumaini."

Kwa Wamalawi wengi, uchaguzi huu utakuwa kama chachu ya nchi kurudi katika  hali ya kawaida tangu machafuko yam waka 2019. Gift Magunda, ambaye ni mkaazi wa Lilongwe amesema kuwa:

"Nina matumaini kwamba tukifanya uchaguzi tena, nchi itarudi katika njia ya kawaida na biashara zitaendelea kikamilifu na labda baadhi yetu ambao mikataba yetu ilifutwa, tutapata ajira zetu."

Karatasi za kupiga kura ziliwasili mjini Lilongwe Malawi kutoka Dubai siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Chanzo: DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW