1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malaysia yaanza kuhesabu kura

Mohamed Dahman8 Machi 2008

KUALA LUMPUR

Wananchi wa Malaysia leo hii wamepiga kura katika uchaguzi ambao yumkini kabisa ukairudisha madarakani serikali tawala ya mseto lakini ambao unaweza ukazusha matatizo kwa uongozi wa waziri mkuu Ahmad Badawi na mvutano wa kikabila katika taifa hilo la makabila mchanganyiko la Kusini mashariki mwa Asia.

Baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura afisa mkuu wa uchaguzi amesema asilimia 70 ya watu milioni 10.9 wenye kustahiki kupiga kura wamepiga kura zao.

Serikali tawala inatazamiwa sana kushinda uchaguzi huo ambao umeitishwa kabla ya muda wake hapo mwezi wa Mei mwaka 2009 na kwa kiasi kikubwa kuonekana kama ni kura ya maoni kwa utawala wa Waziri Mkuu Badawi.

Anwar Ibrahim ni naibu waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha Keadilan Rakyat ambaye amepigwa marufuku kushiriki uchaguzi huo kutokana na mashtaka ya rushwa.

Polisi imepiga marufuku maandamano ya kusheherekea ushindi baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi baadae leo hii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW