SiasaMalaysia
Malaysia yajindaa kwa mazungumzo na China kuhusu bahari
3 Aprili 2023Matangazo
Hayo yameelezwa leo na kituo cha habari cha taifa ambacho kimemnukuu waziri mkuu wa nchi hiyo Anwar Ibrahim.
Suala hilo lilizushwa kwenye mkutano kati ya waziri mkuu huyo na rais wa China Xi Jinping wiki iliyopita,katika wakati ambapo Malaysia imeanzisha mradi wa kutafiti uchimbaji mafuta na gesi katika eneo hilo.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema China nayo inadai eneo hilo ni milki yake na nchi yake ndogo inahitaji mafuta na gesi na kwa hivyo inabidi iendelee na mradi huo. Lakini ikiwa sharti la kufanya hivyo ni kuwepo mazungumzo basi nchi yake iko tayari.
China inadai kuwa na haki ya umiliki wa takriban eneo zima la bahari ya kusini ya China ambalo pia linazozaniwa na Brunei, Ufilipino, Taiwan na Vietnam.