SiasaMalaysia
Malaysia yalenga kuboresha ushirikiano wa ASEAN
19 Januari 2025Matangazo
Malaysia imeandaa mkutano huo kwa mara ya kwanza kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo huku kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoongezeka nchini Myanmar na mivutano katika Bahari ya Kusini ya China.
Soma pia: ASEAN; Myanmar haipaswi kufikiria uchaguzi kwa sasa
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Malaysia Amran Mohamed Zin, amesema wamejitolea sio tu katika kushughulikia masuala ya kikanda lakini pia mgogoro wa Myanmar na k
uendelezwa mazungumzo juu ya Kanuni za maadili za Jumuiya ya ASEAN na China kuhusu eneo la Bahari ya Kusini mwa China.