SiasaMalaysia
Malaysia yampunguzia adhabu Waziri Mkuu wa zamani Najib
2 Februari 2024Matangazo
Najib Razak ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 12 gerezani ataachiwa huru Agosti mwaka 2028, huku faini aliyopewa nayo ikipunguzwa kufikia dola milioni 10 kutoka milioni 50.
Bodi hiyo inayoongozwa na Mfalme wa Malaysia haikutoa sababu za kupunguzwa kwa adhabu hiyo.
Najib alitiwa hatiani kwa ufisadi unaohusishwa na mpango wa maendeleo wa Malaysia 1MDB, ambapo inakadiriwa kwamba dola bilioni 4.5 ziliibwa na nyingine zaidi ya bilioni moja zilihamishiwa katika akaunti zilizounganishwa na waziri mkuu huyo wa zamani.