1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Mali yauonya Umoja wa Mataifa dhidi ya Uingiliaji Niger

24 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop, ameuonya Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake haitakaa kimya iwapo mataifa ya kigeni yataingilia kijeshi nchi jirani ya Niger

Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Septembna 23, 2023
Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye DiopPicha: Mary Altaffer/AP Photo/picture alliance

Diop aliyewakilisha utawala wa kijeshi wa Mali katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa, amesema kuwa Mali bado inapinga vikali uingiliaji wowote wa kijeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS, na kwamba uvamizi wowote nchini Niger unatoa tishio la moja kwa moja kwa amani na usalama wa Mali na hata kwa ukanda huo, hatua aliyosema italeta madhara makubwa.

Diop aikosoa Ufaransa

Diop amesema haya baada ya jeshi la mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso kusaini wiki iliyopita mkataba wa pamoja wa ulinzi.

Soma pia:Viongozi wa kijeshi wa Niger wamkosoa Guterres

Wakati wa kikao hicho cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Diop aliikosoa Ufaransa kwa kile alichosema ni utawala unaojikita katika ukoloni mamboleo huku akiusifia ushirikiano na Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW