Mali: Tumemkata kiongozi wa tawi la IS Sahel
5 Januari 2025Jeshi la Mali limesema vikosi vyake vimewakamata wanaume wawili, mmoja wao akiwa ni kiongozi wa tawi la kundi linalojiita dola la kiislamu IS katika ukanda wa Sahel. Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kwamba imefanikiwa kuwaua wapiganaji kadhaa wa kundi hilo wakati wa operesheni kaskazini mwa nchi hiyo.
Taarifa ya jeshi hilo imesema waliokamatwa ni Mahamad Ould Erkehile almaarufu Abu Rakia" pamoja na "Abu Hash", ambaye imemtaja kuwa kiongozi mwandamizi wa kundi la IS kwenye kanda huyo.
"Abu Hash" anashutumiwa kwa ukatili dhidi ya watu katika maeneo ya Menaka na Gao yaliyopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo pamoja na pamoja na kuratibu mashambulizi dhidi ya jeshi.
Soma pia: Mali yadai kumkamata kiongozi wa IS kanda ya Sahel
Mali imegubikwa na machafuko makubwa tangu mwaka 2012 yanayohusishwa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu IS pamoja na magenge ya wahalifu katika eneo hilo.
Watawala wa kijeshi wa nchi hiyo wamevunja uhusiano na mkoloni wa zamani Ufaransa na kuanzisha uhusiano wa kijeshi na kisiasa na Urusi.