1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mali yadai Algeria inaunga mkono "ugaidi wa kimataifa"

27 Septemba 2025

Waziri Mkuu wa Mali Abdoulaye Maiga ameishutumu Algeria mbele ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa kile alichokiita kuunga mkono "ugaidi wa kimataifa" baada ya kuidungua droni ya jeshi la nchi yake.

Mali imeishutumu Algeria mbele ya Baraza kuu la UN kuwa inaunga mkono ugaidi wa kimataifa
Waziri Mkuu wa Mali Jenerali Abdoulaye MaigaPicha: Bryan R. Smith/AFP

Maiga ameahidi kuwa Mali haitokalia kimya vitendo vya aina hiyo na kuwa italipa kisasi kwa kila ubaya dhidi yake. Ameitolea wito Algeria kuacha kuunga mkono ugaidi wa kimataifa na badala yake ijikite katika kudumisha amani.

Malalamiko ya Mali dhidi ya Algeria mbele ya ICC

Serikali imeshapeleka malalamiko kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, hatua ambayo Algeria imeitaja kuwa ya aibu.

Tangu mwezi Aprili, utawala wa kijeshi wa Mali umekuwa ukilalamika kuwa Algeria iliidungua droni yake madai ambayo hata hivyo upande wa pili umeyakanusha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW