1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yaituhumu Ufaransa kuchafua sifa ya jeshi lake

27 Aprili 2022

Mali imelituhumu jeshi la Ufaransa kwa kile ilichokitaja kuwa "upelelezi" na "upotoshaji" wakati ilipotumia ndege inayoruka bila rubani kupiga picha za kile serikali mjini Paris inadai kuwa ni mamluki waliotenda uhalifu

Mali -Soldaten-Übung
Picha: Ben Curtis/picture alliance/AP Photo

Ufaransa imesema Mamluki hao wanadaiwa kuzika miili ya watu karibu na kambi moja ya jeshi.

Taarifa ya watawala wa kijeshi wa Mali imesema ndege hiyo iliruka kinyume cha sheria katika anga ya kituo cha Gossi mnamo Aprili 20, siku ambayo wanajeshi wa Ufaransa walilikabidhi eneo hilo kwa Mali. 

Siku iliyofuata, jeshi la Ufaransa lilisambaza mkanda wa video iliyosema iliwaonyesha mamluki wa Urusi wakiifukia miili kwa mchanga ili kuwatuhumu wanajeshi walioondoka kuwa walifanya uhalifu wa kivita. 

Mapema jana Jumanne, jeshi la Mali lilitangaza uchunguzi kuhusu kugundulika kwa kaburi la pamoja katika kituo cha kijeshi cha Gossi.

Jeshi hilo limesema Ufaransa inajaribu kuchafua sifa ya wanajeshi wa Mali kwa kutumia video hiyo.

Chanzo: afp