1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yamfukuza balozi wa Sweden

10 Agosti 2024

Serikali ya Mali imemtaka balozi wa Sweden mjini Bamako kuondoka mara moja kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mzozo wa uhusiano wa taifa hilo la Afrika Magharibi na Urusi.

Mali, Niger na Burkina Faso
Viongozi wa kijeshi wa Mali, Assimi Goita, Jenerali Abdourahamane Tiani wa Niger na Kapteni Ibrahim Traore wa Burkina Faso.Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Mali ilitangaza hapo jana kwamba balozi huyo amepewa masaa 72 kuondoka, baada ya Waziri wa Misaada ya Maendeleo na Biashara ya Nje wa Sweden, Johan Forssell, "kutoa matamshi mabaya dhidi ya Mali".

Tayari, Sweden ilikuwa imeshatangaza tangu mwezi Juni kwamba ingeliufunga ubalozi wake mjini Bamako na pia kwenye nchi jirani, Burkina Faso, kufikia mwishoni mwa mwaka huu, na kusitisha misaada kwa mataifa hayo na mengine kadhaa.

Soma zaidi: Ukraine yasikitishwa na kuvunjika uhusiano na Niger

Jumatano iliyopita, Forssell aliandika kwenye mtandao wa X kwamba wanaounga mkono vita vya Urusi nchini Ukraine, wasitarajie kupokea fedha za misaada kutoka Sweden.

Mali imekuwa ikipata msaada wa kijeshi kupitia mamluki wa Kirusi tangu mwaka 2021 na hivi karibuni ilivunja uhusiano wake na Ukraine. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW