1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mali yamfukuza mkuu wa kitengo cha haki za binadamu

6 Februari 2023

Serikali ya mpito ya Mali imemtangaza mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSMA, kuwa ni mtu asiyefaa na kumpa masaa 48 kuondoka.

Mali | MINUSMA | Friedenstruppen | UNPOL
Picha: Nicolas Remene/Le Pictorium/IMAGO

Uamuzi wa kumfukuza Guillaume Ngefa-Atondoko Andali umetokana na uchunguzi wake unaodaiwa kuwa na upendeleo kwa mashahidi na mashirika ya kiraia, kwa ajili ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mali, uliofanyika Januari 27.

Hata hivyo, MINUSMA haijatoa kauli yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya serikali.

Mamlaka nchini Mali zimekuwa zikiandamwa na madai ya ukiukaji wa haki za binaadamu na unyanyasaji unaoripotiwa kufanywa na vikosi vya jeshi la serikali kwa ushirikiano na kundi la mamluki wa kijeshi Urusi, Wagner.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW