Mali yapiga marufuku vyombo vya habari kuripoti siasa
12 Aprili 2024Amri hiyo ilitolewa jana na uongozi wa mamlaka ya mawasiliano na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Katika tangazo hilo, vyombo vyote vya habari ikiwemo vituo vya redio,Televisheni, mtandao na magazeti vimetajwa, ingawa haikufafanuliwa ni kwa namna ufuatiliaji wa hatua ya marufuku hiyo utatekelezwa.
Shirika linalowawakilisha waandishi habari nchini Mali limeipinga hatua ya serikali na kuwatolea mwito waandishi waendelee kuripoti kuhusu masuala ya kisiasa na kusimama imara kutetea haki ya mwananchi ya kupata habari.
Utawala Mali wasitisha shughuli za vyama vya siasa
Mali imekumbwa na mapinduzi mara mbili tangu mwaka 2020 yaliyosababisha hali ya ukosefu wa uthabiti wa kisiasa ambayo imeshuhudiwa pia katika mataifa mengine kadhaa ya eneo hilo la Afrika Magharibi na Kati katika miaka ya hivi karibuni.