Mali yasitisha makubaliano ya amani ya 2015 na waasi
26 Januari 2024Katika taarifa iliyopeperushwa kupitia televisheni, msemaji wa serikali ya Mali Abdoulaye Maiga, amesema utawala wa kijeshi nchini humo umetaja kuweko kwa mabadiliko miongoni mwa makundi yaliotia saini makubaliano hayo ya amani lakini pia "vitendo vya uhasama" vya mpatanishi mkuu, Algeria.
Soma piaMapigano yazuka kati ya waasi wa Tuareg na jeshi la Mali
Maiga amesema serikali ya Mali imebainisha kutowezekana kabisa kutekelezwa kwa makubaliano hayo.
Waasi waliushtumu utawala wa kijeshi kwa kutoheshimu makubaliano
Mnamo Julai 2022, waasi hao wanaotaka kujitenga, walioungana chini ya uratibu wa Harakati za Azawad (CMA), tayari walikuwa wameushtumu utawala huo wa kijeshi kwa "kutotekeleza" makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yaliosimamiwa na Algeria, yalitaka kujumuishwa kwawaasi wa zamani katika vikosi vya ulinzi vya Mali pamoja na uhuru zaidi katika maeneo ya nchi hiyo.