1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yawakamata maafisa 4 wa kampuni ya madini ya Canada

27 Novemba 2024

Maafisa nchini Mali wamewakamata wafanyakazi wanne waandamizi wa kampuni ya madini ya Canada.

Symbolbild | Gold
Madini ya dhahabuPicha: Pond5 Images/IMAGO

Utawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi linaendelea kuwakamata wafanyakazi ili kuzishinikiza kampuni katika sekta yake muhimu ya madini kulipa mamilioni katika kodi za ziada. Kampuni ya Barrick Gold imethibitisha katika taarifa kuwa wafanyakazi wake katika mgodi wa Loulo-Gounkoto wamefunguliwa mashitaka na wasubiri kesi yao baada ya kukamatwa Jumatatu jioni. Kampuni hiyo imesema inapinga mashitaka hayo lakini haikusema ni mashitaka gani. Maafisa wa Mali walikataa kuzungumzia ukamataji huo. Mapema mwezi huu, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Australia ya Resolute Mining na wafanyakazi wawili walikamatwa katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Waliachiwa huru baada ya kampuni hiyo kulipa dola milioni 80 kwa mamlaka za Mali ili kutatua mzozo wa kodi na kuahidi kulipa dola milioni 80 nyingine katika miezi ijayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW