Maliasili duniani itumiwe kwa uangalifu na heshima
25 Desemba 2009Matangazo
Katika hotuba aliyotoa mkesha wa Siku Kuu ya Krismasi Rais wa Ujerumani amesema,utaratibu wa kihaki duniani unapaswa pia kuambatanisha usimamizi bora zaidi katika sekta ya fedha.
Mara nyingine tena Rais Köhler amekosoa na kusema kuwa tamaa ya kubahatisha iliyopindukia ndio iliyosababisha msukosuko wa fedha wa hivi karibuni.
Vile vile amesifu kazi zinazofanywa na mamilioni ya raia wenye utambuzi wa kijamii na wanajeshi wa Kijerumani wanaoshiriki katika tume zilizoidhinishwa na Umoja wa Mataifa katika nchi za ngámbo.