1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Malori ya misaada yaanza kuingia Gaza

19 Januari 2025

Umoja wa Mataifa umesema malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu yameingia Gaza baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza kutekelezwa Jumapili.

Misri Sinai 2025 | Wanajeshi wasindikiza misaada Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.
Malori ya misaada ya kibinaadamu yaanza kuingia katika Ukanda wa Gaza baada makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa.Picha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, afisa mkuu wa muda wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada la OCHA kwa maeneo ya Palestina, Jonathan Whittall, amesema lori la kwanza la misaada ya kiutu limeingia katika Ukanda wa Gaza mara baada ya makubaliano kuanza kutekelezwa.

Soma pia: Usitishaji mapigano waanza kutekelezwa Gaza

Huku haya yakijiri Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ilikuwa muhimu kwa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kati ya Israel na Hamas hatimaye kutekelezwa na hatimaye mateka waliobaki kuachiliwa.

Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis ametoa shukrani kufuatia usitishwaji vita Gaza na kusifu dhima ya wapatanishi waliohusika.

Soma pia: Israel itawaachilia zaidi ya wafungwa 1900 wa Kipalestina

Papa Francis aliwashukuru wote waliohusika katika kufanikisha mpango huo, akiwaombea mateka wote waweze kurudi nyumbani na kuwakumbatia tena wapendwa wao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW