1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malori yachomwa moto katika mashambulizi ya Afrika Kusini

12 Julai 2023

Polisi ya Afrika Kusini imesema kuwa malori 21 yamechomwa moto katika mfululizo wa mashambulizi yenye utata ambayo rais Cyril Ramaphosa ameyataja kuwa matendo ya "uhujumu uchumi".

Russland | Südafrikas Präsident Cyril Ramaphosa in St Petesburg
Picha: Grigory Sysoyev/Sputnik/AP/picture alliance

Hii leo washambuliaji wasiofahamika waliyatia moto malori manne katika jimbo la kaskazini mashariki la Mpumalanga ikiwa ni tukio la hii karibuni kabisa la mfululizo wa matukio hayo yaliyozusha wasiwasi miongoni mwa kampuni za usafirishaji.

Mashambulizi hayo yalianza siku ya Jumapili, wakati wa kumbukumbu ya miaka miwili tangu kuzuka machafuko makubwa ya Julai mwaka 2021 yaliyoanza kwa kuchomwa moto malori. Hujuma hizo zilisambaa na kugeuka machafuko makubwa kuhawi kushuhudiwa nchini humo tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Waziri anayeshughulikia idara ya Polisi Bheki Cele amewaambia waandishi habari mjini Pretoria kuwa wanafahamu uhalifu huo ni wa kupangwa na taarifa za kijasusi zinaashairia yana mafungamano na uhasama wa kibiashara. Kwenye matukio hayo madereva walilazimishwa na watu wenye silaha kuyatekeleza magari yao ambao baadaye waliyateketeza kwa moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW