MALTA:Waafrika 22 wahofiwa kuzama baharini
21 Juni 2007Matangazo
Waafrika 22 wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya chombo chao cha usafiri kuzama katika bahari ya Mediterania kusini mwa Malta. Waafrika wanne walionusurika waliweza kuokolewa kwa mashua ya wavuvi.
Waafrika hao walikuwa njiani katika jaribio la kutaka kuhamia Ulaya ili kujipatia maisha bora .
Waafrika wengine mia moja walikufa maji ama walipotea mwezi uliopita katika bahari, kati ya Libya na Malta.