1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mama, wakili wasema mwili wa Navalny haupo chumba cha maiti

Hawa Bihoga
17 Februari 2024

Mama na Wakili wa mkosoaji wa Ikulu wa kremlin Alexei Navalny aliyefariki katika kifo kinachotajwa cha utata akiwa gerezani, wamesema mwili wake "haupo katika chumba cha kuhifadhia maiti" alipokuwa akizuiliwa.

St. Petersburg | Alexei Navalny
Rambi rambi kufuatia kifo cha Alexei Navalny, mkosoaji wa rais wa Urusi, Vladimir PutinPicha: Dmitri Lovetsky/AP/picture alliance

Kupitia mtandao wa X zamani Twitter msemaji wa Navalny Kira Yarmysh, alithibitisha kifo cha mkosoaji huo na katika chapisho tofauti aliongeza kuwa licha ya kituo cha kuhifadhia maiti cha Salekhard kutofanya kazi siku ya leo, lakini waliambiwa mwili wa mkosoaji huyo haupo katika chumba hicho.

Msemaji huyo aliongeza kuwa, wakili wa Navalny aliwajulisha kwamba sababu ya kifo chake haijajulikana kwa sasa na kwamba mamlaka inakwepa kuukabidhi mwili kwa familia yake.

Kufuatia kifo cha Navalny mataifa ya Magharibi yamemnyooshea kidole cha lawama rais Vladimir Putin na serikali yake, yakimshutumu kuhusika na kifo hicho.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW