1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Mambo magumu kati ya City na Madrid

10 Mei 2023

Magwiji wa soka Manchester City na Real Madrid wametoshana nguvu katia mechi za kwanza za nusu fainali za michuano ya mabingwa Ulaya.

Champions League Halbfinale Real Madrid Manchester City
Picha: Pressinphoto/Lagencia/Imago

Katika kandanda, michezo ya duru ya kwanza ya nusu fainali ya kuwania kikombe cha klabu bingwa barani Ulaya Champions League imefungua pazia usiku wa kuamkia lJumatano kwa mtanange wa kukata na shoka kati ya Real Madrid na Manchester City. Katika mchano huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute magwiji hao wa soka wamelazimishana kutoka sare ya moja kwa moja. Kwa nyakati tofauti washambuliaji Vinícius Júnior na Kevin de Bruyne waliwainua mashabiki wao kwa mikwaju ya mbali. Goli la utangulizi kwa upande wa Madrid liliwekwa kimiani na Vinicius Jr lakini katika nusu ya pili ya mchezo huo Kevin De Bruyne wa City akasawazisha. Duru ya pili itachezwa juma lijalo mjini Manchester.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW