1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia kwa maelfu wakimbia kimbunga Man-yi Ufilipino

16 Novemba 2024

Kimbunga kikali cha Man-yi kinachozidi kuwa na nguvu kinapokaribia Ufilipino kimezusha hofu ya kusababisha maafa, huku mamilioni ya watu wakiwa hatarini kutokana na mawimbi ya dhoruba.

Ufilipino | Uharibifu uliosababishwa na dhoruba ya kitropiki ya Trami(Maktaba)
Zaidi ya watu 650,000 wamehamishwa, kutoka maeneo yaliyoharibiwa na kimbunga Man-yi.Picha: Philippine Coast Guard via AP/picture alliance

Kikiwa na kasi ya upepo wa hadi kilomita 240 kwa saa, kimbunga hicho kinatarajiwa kutua mwishoni mwa wiki hii, kikigusa kisiwa cha Catanduanes na maeneo mengine yanayozunguka kisiwa hicho.

Soma pia: Maelfu wahamishwa Ufilipino wakati kimbunga Man-yi kikaribia

Zaidi ya watu 650,000 wamehamishwa, huku vituo vya uhamishaji vikifurika katika maeneo yaliyoathiriwa kama Catanduanes na Albay. Watu 163 wamefariki kutokana na vimbunga vya hivi karibuni nchini Ufilipino, na serikali inahimiza watu kuhama ili kuepuka hatari.

Wanasayansi wanahusisha kuongezeka kwa nguvu za vimbunga hivi na mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanasababisha mvua kubwa na upepo mkali zaidi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW