1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia waachwa bila makao kufuatia machafuko mapya Haiti

12 Mei 2026

Wimbi jipya la machafuko ya magenge yamepelekea mamia ya watu kuukimbia Mji Mkuu wa Haiti Port-au-Prince.

Moto uliowashwa barabarani kufuatia machafuko Haiti
Moto uliowashwa barabarani kufuatia machafuko HaitiPicha: Arte France

Watu hao wanadaiwa kukita kambi katika barabara inayoelekea uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo.

Hospitali katika mji wa Cite Soleil ziliwahamisha wagonjwa wake na shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka la MSF limesimamisha kutoa huduma zake katika eneo hilo. Machafuko hayo ya magenge yaliibuka mwishoni mwa wiki katika mitaa kadhaa ya mji mkuu.

Polisi inasema kuwa magenge hayo yametanua operesheni zake ikiwemo uporaji, utekaji nyara, udhalilishaji kingono na ubakaji hadi katika maeneo ya vijijini.

Haiti haijawa na rais tangu kuuwawa kwa Rais Jovenal Moise mnamo Julai 2021.

Ripoti iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM mapema mwaka huu ilisema kuwa machafuko ya magenge yamewapelekea watu milioni 1.4 kuyakimbia makaazi yao nchini Haiti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW