1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Mamia ya wahamiaji waokolewa katika pwani ya Italia

12 Machi 2023

Walinzi wa pwani ya Italia pamoja na jeshi la wanamaji wamewasafirisha na kuwapeleka sehemu salama mamia ya wahamiaji waliookolewa.

Italien Crotone, Hafen | Fischerboot mit 500 Migranten, Polizeikontrolle
Picha: Giuseppe Pipita/Zuma/picture alliance

Maelfu ya wahamiaji wengine wameripotiwa kuwasili katika kisiwa kidogo cha watalii katika bahari ya Mediterania.

Katika taarifa, walinzi hao wa pwani wameeleza kuwa msongamano ndani ya meli zilizowabeba wahamiaji hao pamoja na hali mbaya ya hali ya hewa imeathiri shughuli ya uokozi ilioanza siku ya Ijumaa katika bahari ya Lonia karibu na Calabria.

Kuwasili kwa wahamiaji hao kunatokea katikati ya msako mkali unaofanywa na serikali ya mrengo wa kulia ya Italia dhidi ya wasafirishaji haramu wa watu, msako uliotangazwa siku mbili zilizopita.

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa linakadiria kuwa, watu wapatao 300 wamekufa mwaka huu pekee au hawajulikani walipo baada ya kujaribu kuvuka na kuingia Ulaya kupitia njia hatari ya bahari ya Mediterania.